Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu anapenda kuwatangazia wananchi wafuatao kumalizia malipo ya viwanja ambavyo waliuziwa na Halmashauri mwaka 2013 kwa eneo la Ilungu na mwaka 2019 kwa eneo la Igudija kabla ya tarehe 15.12. 2024. Viwanja vya Ilungu vinapatikana eneo la Ilungu sehemu inapojengwa ofisi mpya ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Viwanja vya Igudija vinapatikana Kisesa.
Aidha ikiwa malipo hayo hayatakamilishwa ndani ya siku hizo, kiwanja kitatolewa kwa mwombaji mwingine na hakuna fedha itakayorejeshwa. Mwombaji atakapolipia kiwanja atatakiwa kuwasilisha nakala ya stakabadhi aliyofanyia malipo katika ofisi za Ardhi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu za ofisi sawa.
Pia Mkurugenzi anawatangazia wananchi wote wenye mahitaji ya viwanja kwenye maeneo tajwa kufika Halmashauri ya Wilaya ya Magu kuchagua viwanja kuanzia tarehe 16/12/2024 hadi tarehe 31/12/2024, Mnunuzi atatakiwa kukamilisha malipo ya kiwanja ndani ya siku kumi na nne. Tumia namba hii 0754537854 kwa mawasiliano zaidi.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa