Kusimamia usambazaji wa viuwatilifu pamoja na vinyunyizi vya mazao kwa wakulima.
Kutoa elimu kwa wakulima kuhusiana na mazao yanayotakiwa kulimwa kwenye maeneo yao.
Kufanya utafiti wa hali halisi na upatikanaji wa chakula katika wilaya na kutoa ushauri kwa Serikali.
Kutoa ushauri mbalimbali kwa wakulima kuhusu kuhifadhi chakula na kulima na kulima mazao yanayochukua muda mfupi kulingana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kushauri wakulima kupanda mtama katika maeneo yao kwani unahimili ukame.
Kuhamasisha wakulima kulima zao la pamba ili wajiongezee kipato chao.
Kutoa ushauri mbalimbali kwa wananchi/wakulima kuhusiana na kulima kilimo chenye tija.
Kusimamia miradi mbalimbali inayohusiana na kilimo katika wilaya ili kuleta maendeleo endelevu katika kutoa huduma kwa wananchi.
Kutoa elimu ya ushirika na ujasiriamali kwa viongozi wa vyama vya ushirika.
Kusimamia na kuratibu mikutano mikuu ya SACCOS na AMCOS katika Wilaya.