IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
UTANGULIZI:
Idara ya Mifugo inaundwa na vitengo viwili (2). Kitengo cha Mifugo na kitengo cha Uvuvi. Jumla ya watumishi wa idara ni 55 ambapo kitengo cha Mifugo kina watumishi 43 na kitengo cha Uvuvi kina watumishi 12.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Wilaya ya Magu ina jumla ya ng’ombe 204,250 wa asili, ng’ombe 259 wa kisasa, punda 318, mbuzi 61,007 kondoo 38,645, nguruwe 1,603, mbwa 6560, paka 2460, kuku wa asili 385,557 na kuku wa mayai 18,397.
Kwa mujibu wa Sensa ya Wavuvi ya mwaka 2016, wilaya ya Magu ina jumla ya wavuvi 2708 wenye kumiliki mitumbwi 581 na nyavu 13088. Pia wilaya ina wafugaji wa samaki 110 wenye jumla ya mabwawa 135.
MALENGO YA IDARA
Lengo kubwa ni kuhakikisha wafugaji wanapata Elimu ya ufugaji bora wa kisasa na wenye tija kwa nia ya kumfanya mfugaji aongeze kipato ili aondokane na umaskini uliokithiri lakini pia kuongeza pato la Taifa.
VITENGO VYA IDARA NA MAJUKUMU YAKE
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa