Kutokana na sensa ya mwaka 2012 Halmashauri ya wilaya ya Magu ilikuwa na watu 299,759 kwa kutumia ongezeko la watu 3% inakadiriwa mwaka huu 2017 kuna watu wapatao 318,015 na Idara ya maji yenye vitengo viwili vya maji mjini na maji vijijini hutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi waishio Magu mjini 10,639 kati ya watu 46,256 sawa na asilimia 23 na vijijini ina watu wapatao 271,759 wanaopata maji ni 119,357 sawa na asilimia 43.92 ya idadi ya watu wote waishio vijijini kupitia vyanzo vya maji mbalimbali. Kiwilaya watu wanaopata maji ni watu 129,995 sawa na asilimia 40.88
Miradi ya maji katika wilaya ya Magu.
Miradi ya maji bomba mitano (05) ambayo ni Kisesa, Nyanguge - Muda, Kahangara, Kabila – Ndagalu na Magu mjini (Busulwa).
Matanki ya kuvuna maji ya mvua ni 63, yanayotumika ni 38
Malambo 16.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa