UTANGULIZI:
MAENDELO YA JAMII NI NINI?
Maendeleo ya jamii ni mchakato wa kujenga uwezo wa jamii endelevu, inayojiamini na yenye uwezo wa kujituma na kushiriki kwa misingi ya usawa na kuheshimiana, katika kubaini mahitaji yao. Aidha kubuni, kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango ya kujiletea maendeleo kwa kutumia kikamilifu raslimali za ndani na nje.
Jamii hazifanani na hivyo matatizo ya jamii pia hutofanutiana.
Jamii hutofautiana kutokana na mila, imani, desturi, maadili na historia inayorithishwa kutoka kikazi kimoja hadi kingine na mazingira wanamoishi na kazi zinazowezesha kujikimu. Vigezo hivyo vinaweza kuwa vichocheo au vikwazo katika kuleta maendeleo.
USTAWI WA JAMII NI NINI?
Ustawi wa Jamii ni mchakato wa kujenga jamii kimaadili ili istawi kwa kumsaidia mtu mmoja mmoja mwenye tatizo la kifamilia ambalo linaweza kumsababishia madhara (kijamii, kisaikolojia na kiuchumi) au kikundi cha watu wenye tatizo linalofanana.
Ustawi wa Jamii unategemea zaidi uhiyari wa mhudumiwa na mtaalamu wa ustawi wa jamii kwa kumsaidia kufahamu tatizo alilonalo, kulikabili na kusikiliza ushauri na kuweza kuchukua uamuzi baada ya kushauriwa (kukabili tatizo). Pia mteja anatakiwa kutekeleza na kuyasimamia maamuzi yaliyofikiwa.
KAZI ZINAZOFANYWA:
MAENDELEO YA JAMII.
Kuunganisha nguvu za jamii na serikali ili kuondoa fikra tegemezi.
Kutoa elimu kwa vikundi vya kijamii na kiuchumi kwa njia ya kushiriki maonesho ya biashara na majadiliano.
Kufanya tafiti shirikishi za kijamii na kiuchumi ili kubaini fursa na vikwazo katika kujiletea maendeleo.
Kuimarisha demokrasia ili kuongeza kasi ya maendeleo ya watu.
Kuongoza na kusimamia utekelezaji wa mipango na miradi ya maendeleo.
Kuwezesha viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali kutengeneza ratiba za utekelezaji wa mpango/miradi endelevu ya maendeleo.
Kukusanya, kuchambua, kutafsiri na kutunza takwimu na kumbukumbu mbali mbali kwa ajili ya matumizi ya jamii/serikali na Halmashauri.
Kusimamia na kuratibu shughuli za maendeleo, jinsia na watoto.
Kuratibu masuala ya UKIMWI na athari zake katika jamii.
Kusimamia utekelezaji wa sera mbali mbali.
USTAWI WA JAMII.
Kutoa Huduma kwa Familia na watoto.
Kushughulikia masuala ya usuluhishi wa ndoa.
Kushughulikia matunzo ya mamba/watoto nje ya ndoa.
Kushughulikia matunzo ya mama/watoto katika wahalifu kwenye mahabusu ya watoto.
Kusimamia huduma kwa watoto sugu wanaokwenda shule ya maadilisho.
Kutoa huduma za marekebisho, utengamano na matunzo ya walemavu/wasiojiweza.
Kusimamia huduma za matunzo ya wazee nje na ndani ya makazi.
Kusimamia na kuratibu huduma za marekebisho ya walemavu.
Kutoa huduma za vituo vya watoto wadogo mchana.
Kusimamia na kuhimiza huduma za vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.
Kushughulikia masuala ya watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi kwa kuhamasisha jamii waliyomo kuwaona kuwa ni watoto wao kupitia kamati husika.
SHUGHULI ZINAZOTEKELEZWA NA IDARA.
Uratibu wa mashirika yasiyo ya ki-serikali (NGO`s) na Asasi za kijamii (CBO`s).
Idara inajukumu la kuratibu shughuli za NGO`s na CBO`s na kusimamia utekelezaji wa sera ya Taifa ya NGO`s na CBO`s ya mwaka 2001 na sheria ya NGO`s Na. 24 ya mwaka 2002.
Aidha Idara inajishughulisha na yafuatayo:-
Kuelimisha jamii kuunda vikundi na umuhimu wa kuwa na katiba.
Kushauri na kusimamia uundaji wa katiba za vikundi.
Kuwezesha vikundi kupata elimu ya ujasiriamali.
Kusaidia vikundi kuandaa michakato ya miradi na mikakati ya biashara.
2. kuratibu mfuko wa maendeleo ya wanawake ( W.D.F) na mfuko wa maendeleo ya vijana (Y.D.F) na kutoa mikopo yenye riba nafuu.
Mfuko unatoa mkopo kwa kikundi cha wanawake watono (5) na kuendelea.
Kikundi lazima kiwe na biashara na Akaunt ya Benki.
Kikundi lazima kitambulike katika ngazi ya kijiji na Kata.
Kikundi kiwe na mchanganuo wa mradi unaombewa mkopo.
Kikunndi kiwe na mdhamini
Wanakikundi wawe wanaishi katika kata husika.
Mkopo wa kuanzia ni Tsh 300,000 na ukirejeshwa unaongezewa 100% kwa mkopo unaofuata.
Mkopo unarejeshwa na riba ya 10%.
Mkopo unarejeshwa ndani ya miezi 6.
MFUKO WA MAENDELEO YA VIJANA (Y.D.F).
Jukumu kuu ia sehemu hii ni kuratibu utoaji wa mkopo hiyo kwa vijana katika Halmashauri.
Mikopo hiyo hutolewa na SACCOS baada ya kupata fedha za ruzuku kupitia Halmashauri.
Aidha masharti ya mikopo hiyo husimamiwa na SACCOS husika.
3. Kuratibu Umoja wa Serikali za Mitaa zinazozunguka ziwa Victoria ( LVRLAC).
Lengo kuu la Umoja huu ni kufanya kazi na jamii katika utumiaji wa raslimali za Ziwa Victoria. Shughuli kuu zinazofanywa na umoja huu ni:-
Kutoa mafunzo ya stadi za ujasilia mali na usimamizi wa biashara.
Kutoa mafunzo ya stadi za maisha kwa watoto wa kike mashuleni na nje ya shule.
4. Kuratibu na kushirikiana na wadau katika shughuli za kudhibiti UKIMWI na athari zake katika jamii.
Jukumu kuu ni kushirikiana na wadau katika Halmashauri ili kuongeza uchangiaji wa mawazo, nyenzo, usimamizi, uratibu na utekelezaji wa afua za UKIMWI.
Kutumia kila jitihada katika kupunguza kiwango cha maambukizi mapya na kushughulikia athari zake.
5. Kuratibu shughuli za watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi ( MVC). Lengo ni:-
Kuwatambua watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi katika Halmashauri.
Kuunda kamati za MVC za vijiji na mitaa.
Kushirikiana na wadau katika kuwahudumia watoto kwa kuzingatia mahitaji yao.
DCC-MAGU
HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU
IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Simu: 028 – 2530002
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa