Zoezi la upigaji kura katika jimbo la Magu mkoani Mwanza limeendelea kufanyika kwa amani na utulivu huku wananchi wakiipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa maandalizi mazuri.

Zoezi hilo lilimeanza leo Jumatano saa moja asubuhi na kushuhudia mwamko wa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali ikiwamo kituo cha Magu mjini kilichopo Magu Stend na Itumbili.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao akiwamo John Mambaz ambaye ni mlemavu wa mguu, amepongeza mapokezi na utaratibu wa upigaji kura na kusisitiza kuwa wananchi waendelee kujitokeza kupiga kura.
“Kwa kweli hata mimi mlemavu, nimepokewa vizuri na kushiriki zoezi hili, natoa wito kwa wananchi wenzangu waje wapige kura kwa sababu ni haki yao ya kikatiba,” amesema.

Naye Paschal Robert ambaye ameshiriki zoezi hilo, amepongeza amani na utulivu uliopo kwenye zoezi hilo na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kudumisha amani.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa