Chama cha Madereva wa Halmashauri kimetembelea ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Magu kwa lengo la kujitambulisha rasmi pamoja na kueleza malengo na shughuli wanazozifanya kupitia umoja wao.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama mwenyekiti wa chama hicho Ahmed Salum alieleza kuwa wameamua kuunda umoja huo ili kujenga mshikamano, kusaidiana katika changamoto mbalimbali, na kuwa na jukwaa la kujadili maendeleo yao binafsi na ya taasisi kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Mohamed Ramadhani aliwapongeza kwa hatua hiyo ya kuonesha mshikamano na kuhimiza maadili ya kusaidiana katika raha na shida.

Pia aliwataka kutumia umoja huo kama fursa ya kuanzisha miradi ya uzalishaji mali ili kuongeza kipato cha ziada, akisisitiza umuhimu wa wafanyakazi kuwa na vyanzo mbadala vya mapato.
“Mnapokuwa na umoja kama huu, ni vyema mkautumia vizuri kwa kuanzisha miradi itakayowasaidia kiuchumi. Hii itapunguza utegemezi na kuongeza ustawi wenu binafsi,” alisema Mkurugenzi.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa