Wagombea nane wa nafasi ya ubunge kupitia vyama mbalimbali vya siasa wameendelea kujitokeza katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Magu kwa ajili ya kuchukua fomu za uteuzi wa nafasi ya ubunge.
Katika siku ya jana tarehe 21 na leo 22 Agosti 2025 wagombea ubunge wawili ambao ni Bi Kulwa Makoye Kwangu kutoka Chama cha Wananchi (CUF) na Bi. Lidia Heli Tula kutoka Chama cha DP wamechukua fomu za uteuzi na kufikisha idadi ya wagombe nane waliochukua fomu hizo.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Magu, Mohamed Kyande, kwa upande wa udiwani waliochukua fomu tangu zoezi hilo lianze Agosti 14 mwaka huu, jumla ni 59.
Wagombea hao kutoka vyama mbalimbali vya siasa wamejitokeza kuchukua fomu hizo kuwania nafasi ya udiwani katika kata 25 za jimbo la Magu.
Zoezi la utoaji fomu za uteuzi linatarajiwa kuhitimishwa siku ya Jumatano ya tarehe 27 Agosti 2025.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa