Baraza la madiwani halmashauri ya Wilaya ya Magu limepitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo halmashauri iliomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi Bilioni 73.25 ( Tsh. 73,252,591,128.67) kutoka vyanzo vyake mbalimbali na kutoka ruzuku ya serikali kuu.
Baraza hilo limepitisha mapendekezo ya rasimu hiyo katika kikao maalum cha baraza la madiwani kwaajili ya kupitisha mapendekezo ya rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kilichofanyika leo Alhamisi Januari 29/2026 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.

Akiwasilisha mapendekezo ya rasimu hiyo kwa niaba ya mkurugenzi afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Magu Mophen Mwakajongaamesema bajeti kuu ya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2026/2027 imeongezeka kutoka Bilioni 66.92 hadi Bilioni 73.25 sawa na ongezeko la asilimia 9.4 ukilinganisha na bajeti inayoendelea ya mwaka wa fedha 2024-2025.
Ameongeza kuwa makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka 2026/2027 yameongezeka kutoa shilingi bilioni 6.62 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 hadi bilioni 6.85 sawa na ongezeko la asilimia 3.6.
Akizungumza baada ya kupitisha rasimu hiyo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Mh. Edward Kihamba amesisitiza umuhimu wa halmashauri kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani na kuweka mikakati Madhubuti na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Amesema hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na itasaidia kuboresha huduma za jamii na kiuchumi ikiwemo elimu, afya, miundimbinu na usafi wa mazingira.
Aidha, Mwenyekiti huyo amewataka Madiwani kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao na kuhakikisha miradi yote iliyopangwa inakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa, ili wananchi wanufaike na fedha zinazotolewa.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Ramadhani amesisitiza kuwa halmashauri hiyo itazidi kuongeza ufanisi wa matumizi ya mifumo ili kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Amesema mifumo hiyo ni pamoja na GoT-HOMIS -ni mfumo wa kilectroniki ulianzishwa kwaajili ya usimamizi na uendeshaji wa vituo vya kutole huduma za Afya.
Amesema ili kuboresha utendaji kazi miongoni mwa watumishi, kuanzia juzi tayari halmashauri imeanza kutumia mfumo wa matumizi ya mfumo wa ofisi mtandao (e- office) utasaidia kupunguza gharama za kiundeshaji.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa