Mkuu wa wilaya ya Magu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya MH:Salum Kalli akiwa Pamoja na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya bi fidelica myovella ,Mganga mkuu wa wilaya Dr Maria Kapinga wameshiriki kukagua baadhi ya miradi ya afya inayotekelezwa kutokana na nguvu za wananchi,halmashauri ya wilaya Pamoja na ile inayotekelezwa na serikali kuu baadhi ya miradi hiyo ni zahanati ya igombe kata ya kabila iligharimu shillingi million 50 ikiwa ni mchango wa nguvu za wananchi Pamoja na mapato ya ndani ya halmashauri mradi mwingine ni kituo cha afya shishani kilichogharimu tsh miliono 500 ikiwa nifedha toka serikali kuu kutokana na tozo za miamala ya simu aidha ametembelea kituo cha afya cha kahangara,zahanati tarajiwa za muda na salong’we Pamoja na kituo cha afya kisesa ambapo katika zahanati ya kahangara amekagua na kupata maelezo yam ashine mpya na kisasa ya mionzi x-ray inayoweza kupima wagonjwa 360 kwa siku na kutunza kumbukumbu kwa muda wa miaka mitano katika kituo cha afya kisesa kamati hiyo imekagua mashine inayotumika kupima damu,mapigo ya moyo presha wakati mgonjwa akifanyiwa upasuaji
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa