Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu bw SIMON MPANDALUME leo tarehe 14/02/2022 ameongoza Kamati ya uongozi na fedha ya Halamashauri hiyo katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kutokana na fedha toka serikali kuu na zile za mapato ya ndani katika ziara hiyo kamati hiyo imetembelea miradi mbalimbali Iliwemo jengo la OPD katika zahanati ya shishani iliyopo kata ya shishani kwa Tsh mill 250 na Shule ya sekondari mpya Nyantimba iliyopo kata ya Buhumbi Tsh 12,500,000 fedha zote hizi ni gawio toka tozo za miamala ya simu toka serikali kuu, lakini pia shule mpya ya seondari Nkunguru iliyopo kata ya Nkunguru Tsh mill 50. Miradi hiyo yote ipo katika hatua mbali mbali za ukamilishaji.
Aidha bwa mpandalume pamoja na kupongeza kamati za ujenzi katika maeneo hayo amesisitiza ukamilishaji wa miradi hiyo ufanyike kwa haraka ili ianze kutumika kwa haraka iwezekanavyo.
Katika ziara hiyo kamati hiyo pia imetembelea kituo cha makumbusho ya kihistoria kilichopo Kijiji cha kageye kata ya Lutale katika eneo hilo kamati ilipendekeza kuboreshwa kwa miundo mbinu yake ili kitumike kama chanzo cha mapato na ajira kwa Halmashauri
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa