Naibu Waziri wa maendeleo ya jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum Mh. Mwanaidi Ali Khamis amevipongeza vikundi vya michezo vya Simba na Yanga katika kijiji cha Nyang'anga kata ya Sukuma wilayani Magu kwa kushirikiana katika amsha ari ya ujenzi wa nyumba bora za makazi zinazojengwa na wananchi kupitia mfumo wa kijamii wa kushirikiana katika kazi.
Naibu Waziri Mwanaidi ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyang'hanga kata ya Sukuma wilayani Magu katika mkutano wa hadhara ambapo alikagua na kushiriki katika amsha ari ya nyumba za wanachi zinazojengwa kwa mfumo wa kijamii wa kushirikiana katika kazi .
Akizungumza na wananchi hao Naibu Waziri Mwanaidi amesema Wizara inafanya Kampeni ya Makazi Bora katika Mikoa mbalimbali kwa kushirikiana na Mikoa na Halmashauri ambapo kuanzia Julai 2022 hadi Aprili 2023 jumla ya nyongeza ya nyumba 732 zilijengwa kwa hamasa ya Kampeni hiyo na kufikisha jumla ya nyumba 5712.
" Ushabiki wa mpira sio michezo tu nimehamasika sana na wakazi wa kijiji hiki kwa kushirikiana katika kuaamsha ari na kushiriki katika ujenzi wa nyumba bora nawapongeza sana kwa mbinu hizi naomba muendelee na umoja huu" amesema Waziri Mwanaidi.
Aidha Naibu Waziri Mwanaidi amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii kuwasikiliza wananchi katika maeneo yao ili kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali wanazokabilia nazo katika jamii ili kuendeleza juhudi za serikali kuwainua wananchi kiuchumi.
" Endeleeni kufanya kazi ya kuwatembelea wananchi vijijini na kutoa elimu kwani mmeajiriwa kwaaji ya kufanya kazi hiyo sio tu kukaa ofisini , tunataka kuona maafisa maendeleo ya jamii wanafanya kazi zao za kuhamasisha wananchi kwa kuwapa yanayohusika na maendeleo ya jamii zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Magu Rachel Kasanda amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yameshirikiana na Serikali kufanya kazi kubwa ya kuingia kwenye Jamii kwa kutoa elimu katika kuonana changamoto mbalimbali ikiwemo kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na kuboresha makazi katika maeneo yao.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa