Leo Ijumaa Agosti 15, 2025 Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa ( JKT) Mh. Dkt. Stargoma Tax amehitimisha mafunzo ya awali ya jeshi la akiba Mkoani Mwanza wilaya ya Magu ambayo yamefundishwa kwa muda wa wiki 18 kuanzia Mwezi Aprili mpaka Mwezi Agosti.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo katika uwanja wa Mwanankanda Kata ya Magu Mjini Wilayani Magu Waziri Tax amewataka vijana kutumia vyema vipaji walivyo navyo ili waweze kujitengenezea ajira na kujiendeleza kiuchumi.
Amesema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa taifa kwani yanawandaa na kuwajengea vijana uwezo wa kulinda amani pamoja na kulinda amani ya taifa.
Kwa apande wake mkuu wa wilaya ya Magu Mh. Jubilate Lawuo ambaye alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri wa kulinda amani na usalama wa wilaya.
Vilevile amewataka vijana hao kutumia fursa mbalimbali za uzalishaji mali zinazopatikana wilayani ili kujikwamua kiuchumi na kujenga uchumi wa nchi.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa