Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya magu tarehe 17.02.2018 ambapo ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha LAKAIRO Kilichopo katika kijiji cha Isangijo. Amepongeza juhudi zinazoonyeshwa na watanzania katika kuanzisha viwanda na kuendana na sera ya “Tanzania ya viwanda” amesisitiza watanzania waendelee kuwekeza katika viwanda kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mali ghafi na kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja kwani kwa kufanya hivyo watu wenye taaluma mbalimbali watapata ajira katika viwanda hivyo.
Akiwa katika kijiji hicho cha Isangijo amesikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wananchi zinazohusu elimu, Afya, maji na miundombinu ya Barabara. Kuhusiana na kero hizo ametoa maagizo kwa viongozi husika ili zitatuliwe.
Aidha ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya kituo cha afya kahangara. Amepongeza uongozi wa Halmashauri kusimamia ujenzi wa majengo yote ya kituo cha afya Kahangara hadi kukamilika kwani ujenzi huo ni mfano wa kuigwa hapa nchini. Amesisitiza Halmashauri ijipange kuhamasisha wananchi ili waanzishe ujenzi wa zahanati katika vijiji ambavyo havina zahanati ili kuboreha huduma za afya katika maeneo yote.
Ameeleza kuwa, Serikali imeleta fedha Tshs 500,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Lugeye, amesema fedha hizo zisimamiwe vizuri zitumike kujenga Maabara, chumba cha upasuaji, wodi ya akina mama, kununua vitanda vya wodi ya akinamama. Pia amezungumza na watumishi ambapo, amesisitiza watumishi wa Umma kuhudumia wananchi na kutatua kero zao kwa wakati.
Amehakikishia watumishi kuwa maslahi yao yanaendelea kufanyiwa kazi na serikali hivyo haina budi watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kuhudumia wananchi kwani serikali inatambua umuhimu wao. Amepata fursa ya kutembelea shamba la mfano la kilimo cha pamba katika kata ya Buhumbi Wilayani Magu ambapo amepongeza juhudi zinazoonyeshwa na wananchi katika kilimo cha pamba.
Shamba la Mfano la kilimo cha Pamba kata ya Buhumbi (chanzo: ziara ya waziri Mkuu)
Kiwanda Cha LAKAIRO kilichopo kijiji cha Isangijo (chanzo: Ziara ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu akikagua Kituo cha Afya Kahangara (Chanzo: Ziara ya Waziri Mkuu)
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa