Halmashauri ya Wilaya ya Magu imefanikiwa kutoa huduma ya matibabu bure kwa Wazee 25499 kwa mwaka 2018, haya yamejiri katika hafla ya kukabidhi vitambulisho vya Matibabu bure kwa wazee wilayani iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Magu. Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Dr. Philemon Sengati akiwa ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya kukabidhi vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee 300 ambao vimetolewa mwezi huu na Halmashauri ya Magu, amesema kuwa takwimu za mwaka 2018, zinaonesha wazee 18315 wakazi wa Magu walipatiwa huduma ya matibabu bure na 7184 waliapatiwa wakitokea katika wilaya za jirani au nje ya Wilaya ya Magu.
DC Sengati pia amekabidhi fimbo nyeupe tano kwa wasioona, kati ya 426 walemavu wasioona walioko katika Wilaya ya Magu, aidha amesisistiza kuwa Wazee wote wawe na amani katika Serikali hii ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt.John Magufuli iko kwa ajili ya kutetea haki, usawa na kuwakwamua wanyonge “Wazee wangu kwa lolote linalowasibu karibuni sana Ofisi yangu, ya DAS na DED ziko wazi kwa ajili ya kuwasililiza na kuwahudumia, pia ninasisitiza kuwa hakuna haja ya kuendelea kukalishwa kwa muda mrefu kusubiri huduma za matibabu hospital ndiyo maana tunalo dirisha la dawa na chumba cha huduma ya tiba kwa wazee. Lengo ni kuwaenzi wazee wetu kwani hata sisi ni wazee watarajiwa” ‘amesema Dkt. Sengati.
Aidha DC Sengati amesema kuwa faida ya kuwa na Rais Mzalendo anayetekeleza miradi mingi, ahadi za ukweli na anayeziishi ahadi zake za ukweli , “hakika mnaona anavyopambana katika kujenga miradi mikubwa, miundombinu ya barabara, madaraja na reli, moja ya faida ni hii ya ninyi kupatiwa huduma ya matibabu bure! kwa sisi wawakilishi wake tunamuunga mkono na tunamkubali naamini hata ninyi wazee wangu mtakwenda kuwa mawakala wazuri wa Serikali yenu inayowajali bila ubaguzi, aidha wa kidini au kisiasa”.
Naye Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Magu Lutengano Mwalwiba amesema kuwa huu ni mwendelezo wa Halmshauri kutoa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee," Lengo ni kwamba tunahitaji kila anayefikia umri wa miaka sitini apate kitambulisho na aanze kupatiwa huduma ya mataibabu bure, na Matarajio yetu ni kuona wazee wote mnapatiwa huduma bure kama ilivyo sera ya Serikali, kuwa wazee mnayo haki ya kupatiwa huduma bure na sisi tunaendelea kutekeleza kama ilivyo kusudiwa na Serikali".
Wazee waliopatiwa vitambulisho wamepongeza jitihada za Serikali, “Kweli Serikali imetukumbuka na sisi Wazee kwani huduma ya tiba ni jambo la muhimu sana kwetu wazee, tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuliona hili na sisi tunamuunga mkono na kwamba bado tunaimani naye na Serikali yake pamoja na Wasaidizi wa Rais, Pia tunamshukuru Dr. Maduhu mganga mkuu wilaya na watoa huduma kwa kutujali pale tunapoenda kupata matitabu katika Hospital ya Wilaya pamoja na vituo vya afya” amesema Mzee. Helmenegild Mganga.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa