Kiswahili
  • English
  • Kiswahili
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MAGU DISTRICT COUNCIL
MAGU DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Magu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Orodha ya viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu Wa Wilaya
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo , umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Utumishi na utawala
      • Idara ya Mipango
      • Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Fedha
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Tehama
      • Internal Audit Unit
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kivutio cha Utalii
      • Bujora
    • Miundombinu ya Umwagiliaji
  • Huduma
    • Afya
    • Maji
    • Elimu
    • Kilimo
  • Madiwani
    • Baraza la Madiwani
      • Wajumbe wa Baraza la Madiwani
      • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya UKIMWI (CMAC)
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba ya vikao vya Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Bajeti
      • 2016/2017 Budget
    • TASAF
    • Mpango Mkakati
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • sheria
    • Fomu mbalimbali
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari

WARATIBU MIKOPO 10% HALMASHAURI MAGU WAPATIWA MAFUNZO

Posted on: October 9th, 2024

JUMLA ya makatibu 25 wa kamati za huduma ya mikopo ngazi ya kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu pamoja na maofisa maendeleo ya jamii 10 ngazi ya wilaya, wamepatiwa mafunzo ya usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri huku wakisisitizwa kuzingatia kanuni na mwongozo katika utoaji wa mikopo hiyo kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Mafunzo hayo ya siku mbili, yameanza kutolewa leo tarehe 9 Oktoba, 2024 katika ukumbi wa Shule ya Msingi Itumbili mjini Magu mkoani Mwanza kwa lengo la kuwawezesha washiriki hao kuwa wasimamizi pamoja na kuhamasisha vikundi vyote kuhusu utoaji wa mikopo hiyo.

Mkufunzi wa mfunzo hayo ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii anayeratibu mikopo vijana, wanawake na watu wenye ulemavu katika halmashauri ya wilaya ya Magu, Shida Missana amesema katika halmashauri hiyo ya Magu wanatarajia kutoa mikopo ya Sh milioni 889.9.

“Mikopo hii ilisimama mwaka jana lakini mwaka huu tumekuwa na muongozo mpya wenye kanuni mpya hivyo tunapitia muongozo pamoja na kanuni zote ili wasimamizi hawa wawe tayari kwa ajili ya kuhamasisha vikundi, kuunda vikundi pamoja na kuwaongoza katika suala zima la kuomba mikopo hii ambayo ni asilimia 10 za mapato zinazotengwa na halmashauri.

“Kwa upande wa Magu tumepata Sh milioni 889.9 na kwa sasa tupo kwenye maandalizi ili kuanzia mwezi Novemba mwaka huu tuanze kutoa mikopo,” amesema.

Amewaasa wasimamizi hao kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa kwa vikundi vya wajasiriamali au vikundi vyenye mawazo ya  kijasiriamali ili kuwezesha makundi yaliyolengwa kujikwamua kiuchumi.

Amesisitiza kuwa makundi ya watu wenye ulemavu yanatakiwa kuwa na watu kuanzia wawili kuendelea huku makundi ya vijana na wanawake wakitakiwa kuwa na watu wasiopungua watano.

“Maombi ya mikopo hii inatakiwa kuwa imechakatwa na kukamilika ndani ya miezi miwili,” amesema, Missana.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili, Abubakari Msere ambaye pia ni afisa maendeleo ya jamii katika halamshauri hiyo, aliushukuru uongozi wa halmashauri hiyo kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo amesema yatakuwa chachu kwao katika usimamizi dhabiti wa mchakato mzima wa utoaji wa mikopo hiyo na kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza.

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA YA WAANDISHI NA WAENDESHA VIFAA WALIOTEULIWA KATIKA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA II April 28, 2025
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU ENEO LA ILUNGU NA IGUDIJA TAREHE 02/12/2024 December 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA November 18, 2022
  • FOMU ZA KUJIUNGA SHULE YA WASICHANA YA MKOA WA MWANZA MWANZA GIRLS SS 2023 December 16, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • KILIO CHA MAJI MWAMABANZA KUISHA JUNI 2025

    May 16, 2025
  • WADAU WA SANAA MAGU WATAKIWA KUJISAJILI BASATA

    May 07, 2025
  • INEC YARIDHISHWA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA MAGU

    May 03, 2025
  • DC Magu:Wazazi pelekeni watoto wapate chanjo ya polio

    April 30, 2025
  • Angalia zote

Video

Serikali yatoa Matrekata 33 katika Halmashauri ya Wilaya ya Magu
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • Fomu ya Kusafiri nje ya Kituo cha kazi
  • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Fomu ya Opras
  • Fomu Mpya ya Maombi ya Likizo kwa watumishi
  • Fomu ya Quotation ya likizo
  • Taratibu za mikutano na uendeshaji shughuli za Halmashauri
  • Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mwanza
  • Utaratibu wa kutoa Leseni ya Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Wakala ya Serikali Mtandao.
  • Wizara ya Afya
  • Tamisemi
  • Utumishi
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti kuu ya serikali
  • Ofisi ya Taifa ya takwimu Tanzania
  • tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa