Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa, Khadija Nyembo azindua sherehe za wiki ya Maji Duniani katika viwanja vya Mkapa vilivyopo Kata ya Kisesa tarehe 16.03.2017. Aidha alianza kwa kuzindua kituo cha Kusukuma Maji Kisesa – Kanyama ambapo aliwashukuru Viongozi wa MWAUWASA, Mkoa na Wilaya kuwahisha mradi wa maji Kisesa kama ulivyokuwa umepangwa kwani mradi huu utapunguza uhaba wa maji katika kata za Kisesa na Bujora. Amesisitiza Wananchi wa Kisesa kutunza vyanzo vya maji na kuhakikisha usafi wa mazingira katika vyanzo vyote. Pia ameonya wananchi waepuke kujiungia maji bila kufuata utaratibu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa