Kamati ya lishe Halmashauri ya Wilaya ya Magu leo tarehe 4 Septemba, 2025 imefanya kikao maalum cha tathmini ya utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha April hadi Juni, 2025 ambapo pamoja na mambo mengine jumla ya wajawazito 24,648 wamepatiwa elimu juu ya matumizi ya vidonge vya kuongeza wingi wa damu.
Akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi hicho, Afisa Magdalena Lema amesema wajawazito hao walipata madini ya chuma lron folic Acid (IFA) sawa na asilimia 100.
Amesema halmashauri ya wilava va Magu kupitia Divisheni ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe imekuwa ikitekeleza afua mbalimbali za lishe katika kuhakikisha inaepukana na tatizo la utapiamlo na udumavu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
“Shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na matibabu ya utapiamlo mkali kwa watoto 9 wenye utapiamlo mkali na kupona kabisa sawa na asilimia 100.
“Kutoa elimu ya lishe na kufanya tathimini ya lishe katika kaya zenye watoto chini ya miaka 5, wanawake wajawazito na wanaonyonyesha kwa kupitia wahudumu ngazi ya jami. Jumla ya wazazi/walezi wa watoto chini ya miaka 5. Wazazi/walezi 32,005 sawa na asilimia 100 walipata elimu ya lishe,” amesema.
Awali akiendesha kikao hicho, Kaimu Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu, Eusebius Chanjali ametoa wito kwa jamii na wajumbe wa kamati kuendelea kutoa elimu ya lishe na ulaji bora unaofaa kwa kuzingatia makundi sita ya vyakula hususani kwa mama wajawazito, mama wanaonyonyesha na wazazi/walezi wa watoto chini ya miaka 5.
“Kwa sababu tunaweza kuwa tunavutana na walimu kuhusu maendeleo ya ufaulu wa watoto wetu bila kujua kuwa tayari watoto wana tatizo la udumavu wa akili unaotokana na kutopatiwa lishe bora,” amesema.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa