Shule mpya ya Sekondari ya wasichana Mwanza ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi Bilioni 3 kwa awamu ya Kwanza imeanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano kwaajili ya mwaka mpya wa masomo 2023.
Mkuu wa Wilaya ya Magu Rachel Kassanda aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Magu Bi Fidelica G. Myovella walifika shule hiyo iliyopo Kijiji cha Ihushi Kata ya Bujashi, Wilayani Magu Mkoani Mwanza kwaajili ya kukagua maendeleo ya kuripoti wanafunzi waliopangiwa shuleni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua maendeleo ya kuripoti wanafunzi wa kidato cha tano shule hiyo DC Kassanda amewahimiza wazazi wa wanafunzi ambao hawajaripoti shule kuwapeleka mapema ili waanza masomo kwa wakati na kupata muda wa kuzoea mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Bi. Fidelica G. Myovella ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hssan kwa kutoa fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo hususani katika sekta ya Elimu na afya , katika kupunguza changamoto zinazowakabili wananchi.
Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mwanza umeingia katika awamu ya pili mara baada ya Serikali kutoa zaidi ya Shilingi Bilioni moja kwaajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule ikiwemo Maktaba,Mabweni manne, chumba cha kompyuta na nyumba nne za walimu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa