Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mheshimiwa Josephat Kandege amesema hayo kwenye ziara aliyofanya wilayani Magu tarehe 28.02. 2020 wakati akizungumza na watumishi wa Umma katika ukumbi wa Shule ya sekondari Magu. Amesema kuwa wakopeshaji hao wasio rasmi wamekuwa wakichukua kadi za watumishi na kutumia mikataba ya ulaghai.
Amepongeza Halmashauri ya Magu kupeleka watumishi 6 wa Idara ya afya masomoni, kuanzisha mfuko wa elimu, kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba na kidato cha sita na walimu waliojitolea kujenga darasa kwa fedha zao ambapo amesema kuwa huo ni uzalendo mkubwa ulioonyeshwa na walimu hao.
Aidha amesema “ili Halmashauri ipate maendeleo watumishi lazima wapate ari ya kufanya kazi kwa bidii na ili Halmashauri iweze kujiendesha Lazima kuzingatia ukusanyaji wa Mapato na watendaji wa Kata na vijiji wawe wasimamizi kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanakusanywa” amesema Naibu waziri OR-TAMISEMI.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Magu Dkt Philemon Sengati amemshukuru Naibu Waziri kutembelea Magu na kuzungumza na watumishi, “Magu tumeamua kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa na mshikamano na tunazingatia rasilimali watu” amesema Dkt Sengati.
Mbunge Jimbo la Magu Mhe. Destery Kiswaga amesema kuwa watumishi wana changamoto nyingi serikali ikiendelea kuzipunguza watakuwa na molari ya kufanya kazi. Pia Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Hilali Elisha amesema wananchi wa Magu wamehamasika sana katika kuinua maboma ya Madarasa na zahanati katika suala la kuleta maendeleo ameomba serikali kusaidia nguvu za wananchi kwa kuezeka maboma yaliyopo.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Bw Lutengano G. Mwalwiba amesema kuwa serikali imeendelea kushughulikia changamoto za watumishi kwa wakati kwani changamoto kubwa iliyopo ni upandishaji wa madaraja kwa watumishi. Mwaka 2019 serikali ilitoa kibari cha kupandisha watumishi lakini waliobadilishiwa mshahara ni watumishi 411 bado watumishi 74 ambao hawajabadilishiwa mshahara hivyo ameomba Serikali kuwabadilishia mshahara watumishi waliobaki katika Halmashauri ya Magu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa