Mkurugenzi mtendaji wa Mji wa Mafinga Bi. Fidelica G. Myovella amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yaMagu , Mohamed Ramadhan leo Jumamosi Machi 16, 2023 mara baada ya uhamisho uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ; machi 09, 2024 ambapo alimuhamisha Bi Fidelica kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga huku Mohamed Ramadhan akihamishwa kutoka Wilaya ya Nsimbo kuja Magu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya ofisi Bi Fidelica Myovella amewashukuru watumishi wa Wilaya ya Magu kwa ushirikiano waliotoa kipindi chote cha uongozi wake huku akiwasisitiza kutoa ushirikiano huo kwa mkurugenzi Ramadhan.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhan amesisitiza ushirikiano kwa watumishi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Wilaya ya Magu.
Aidha Mkurugenzi Ramadhan amesema yupo tayari kufanya kazi na watumishi na kuwatumikia wananchi wa Magu bila kuchoka kuhakikisha anaendeleza pale alipoishia Mkurugenzi Myovella.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa