Mkuu wa Wilaya ya Magu Mwalimu Khadija Nyembo ameitaka Jamii kuhakikisha inasimamia malezi na makuzi ya watoto vizuri wakati Taifa likiwa linaekea katika Uchumi wa Viwanda. Ameyasema hayo leo Juni 20, 2018 katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Wilayani Magu, yaliyofanyika katika Kata ya Itumbili, ambapo alikuwa mgeni Rasmi katika maamizisho hayo. Nyembo ameitaka jamii kuhakikisha kuwa Watoto wetu wanakua na kulelewa vizuri ili waweze kuielewa dhamira njema ya Serikali ya awamu ya tano iliyoamua kuamsha viwanda katika Taifa kwa lengo la kukuza ajira na stadi za kazi kwa kuifanya Tanzania kuwa Taifa la Viwanda hivyo maadili mema yanahitajika ili kuwandaa watalaam wenye weledi na Uzalendo.
Awali Watoto walisoma Risala kwa Mkuu wa Wilaya iliyaoanisha changamoto zinazowakabili watoto wilayani magu, ikiwemo Ulinzi wa Mtoto, kukatishwa masomo, Kuletekezwa na wazazi, Ukosefu wa mabaraza ya watoto, Vilabu vya watoto Shuleni, Ajira za utotoni, Ukosefu wa maeneo ya michezo, Vitendo vya udhalilishaji, unyanyasaji vinavyopelekea kwa watoto kushindwa kufikia ndoto za maisha yao ya baadaye.
Naye Mgeni Rasmi Mhe.Khadija Nyembo amewahakikishia wananchi na watoto kwa ujumla kuwa, Serikali haitafumbia macho vitendo vyovyote, au mtu yeyote atakayejaribu kuharibu au kukiuka sheria na haki ya mtoto. Sheria itachukua mkondo wake dhidi ya mtu huyo. Na kwamba anahitaji kuona maadili mema kwa watoto yakidumishwa na kuheshimiwa katika jamii. Pia ametoa mwelekeo kuwa Serikali tayari imeshaanza utaratibu wa Kuanzisha mabara ya watoto kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya, Vikundi vya ulinzi wa mtoto, Utoaji wa elimu ya haki ya mtoto na utoaji taarifa pale panapotokea ukiukaji wa haki za mtoto program hii Serikali inashirikiana na Shirika la watoto Duniani (UNICEF).
MKuu wa Wilaya pia amewashukuru Wananchi, Wazazi/Walezi na Vituo vya kulelea watoto waliohudhuria na kuaonesha shughuli mbalimbali za Stadi kazi wanazofundisha kwa watoto, Compassion AICT-Magu, Ilungu, Lugeye, Nyanguge, PF(Pathfinder-SDA Magu) na ELCT-Magu ambao wameonesha stadi za ufundi mbalimbali wanazofundisha kama Ufundi Umeme, Ufundi Ujenzi, Ufundi Seremala, Ushonaji na ufumaji, Ushonaji viatu, Uokaji wa mikate na maandazi,” hii ndiyo Tanzania ya viwanda tunayoitaka” Nyembo alishuwakuru na kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano kwa mfano mzuri walioonesha kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano kuelekea Uchumi wa Viwanda na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema "KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TUSIMUACHE MTOTO NYUMA" Amesisitiza Nyembo.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Magu, Bwana Fundikira Said ameitaka jamii kuendelea kushirikiana na Watoto kwa karibu zaidi katika kuhakikisha kuwa tunabaini na kutatua changamoto au matatizo ya watoto wetu kwa wakati, pia kuhakikisha kuwa jukumu la kulea mtoto ni la mzazi au mlezi hivyo, hatuhitaji kuona watoto wakikatishwa masomo, aidha kwa kuozeshwa, au kuzurura mitaani.
Afisa Maendeleo Bi,Shida Misana amefafanua kuwa dhana ya Viwanda ni fikra zaidi ya majengo. Hivyo akatoa wito kwa jamii kushiriki kikamilifu katika kuwalea watoto kwa kuwapa elimu zaidi kuwa VIWANDA ni kuongeza thamani ya kile unachozalisha, Pia amesisitiza kuwa Elimu ya Kujitegemea na Ufundi inahitaji kuongezewa kasi ya kufundishwa shuleni ili kuwaandaa watoto katika kuelekea Tanzania ya Viwanda.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa