Mkuu wa Wilaya ya Magu Mheshimiwa Dkt. Philemon Sengati (PhD) akiwa ni Mgeni rasmi amezindua mradi wa kuboresha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula (LDFS) unaotekelezwa katika Kata ya Sukuma wilayani Magu. Mradi huu unatekelezwa katika Wilaya tano hapa nchini Tanzania na Magu ikiwemo. Katika Bara la Afrika unatekelezwa katika nchi kumi na mbili tu ambazo ni Kenya, Burundi, Uganda, Ethiopia, Malawi, Switzeland, Nigeria, Ghana, Bukinafasso, Niger, Senegal na Tanzania
DC Sengati amewataka wananchi kuachana na mazoea ya kuharibu mazingira kwa kukata miti ovyo na kuharibu vyanzo vya maji na uoto wa asili, vitendo hivi visipodhibitiwa Nchi yetu itageuka kuwa jangwa, Akimnukuu Mwaasisi wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alipata kusema mapema kuwa “Ili Nchi inedelee inahitaji Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi” “Mimi ninasema kupitia Mwaasisi ardhi, inatakiwa kuhifadhiwa na kutunzwa na maliasili zake kulindwa na kutumika kwa tija kwa ajili ya kizazi kijacho”.
Awali mratibu wa mradi Bwana Ngussa Buyamba ametoa taarifa ya mradi ambapo amedai kuwa Lengo kuu la mradi ni kuboresha usalama wa chakula na lishe katika Vijiji vya Lumeji, Iseni na Nyang’hanga. Huku akitaja kuwa madhumuni ya mradi ni kupunguza uharibifu wa ardhi na kuongeza uzalishaji wa chakula kwenye maeneo yenye mifumo ya nusu jangwa Tanzania,
Walengwa wa mradi ni Wakulima, wafugaji wadogo wasio na uhakika wa chakula, Wenye uhakika wa chakula na wanaozalisha chakula kwa ajili ya biashara wanaolenga mahitaji ya soko. Huku akitaja kuwa njia zitakazoatumika ni kuihamasisha jamii kufuga mifugo kulingana eneo, Upandaji wa miti na uhifadhi wa uoto wa asili, Kilimo hifadhi na vyanzo vya maji.
Bwana Buyamba ameelezea kuwa mradi huo unaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa hisani ya Mfuko ya Mazingira wa Dunia (GEF-Global environment Facility) kupitia mfuko wa kimataifa wa Maendeleo ya kilimo (IFAD).
Wananachi wamepokea mradi huo kwa matumaini makubwa akizungumza kwa niaba ya walengwa Ndugu Erenest Ngolyo mkazi wa Galamugi-Nyang’hanga amesema kuwa Serikali imetenda haki kuwapatia mradi huo kwani utaongeza thamani ya uzalishaji wa chakula na kuwaongezea wananchi kipato na kuwa na ziada ya chakula.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa