JSI imekabidhi vitendea kazi hivyo ili kuboresha utendaji kazi na ufanisi wa wasimamizi wa mashauri ya watoto ikiwa ni pamoja na kurahisisha usafiri na hivyo kuwafikia wasimamizi wa mashauri ya watoto (CCW) wengi zaidi na kutunza kumbukumbu za watoto walio katika mazingira hatarishi na waliopata huduma kwa kipindi husika.
JSI kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Magu Kupitia Mradi wa kubaoresha mifumo ya Afya na ustawi wa Jamii ilifanya mafunzo ya siku 5 mfululizo kwa wasimamizi wa mashauri ya watoto (CCW) katika kata 7 za Halmashauri ya Wilaya ya Magu ili kuchangia kufikia lengo kuu la PEPFAR 3.0 la kufikia 90-90-90 ifikapo mwaka 2020 na lengo la Serikali Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la Sifuri 3 ifikapo mwaka 2030.
Mwakilishi kutoka JSI ameeleza kwamba, Kupitia ushirikiano uliopo baina ya Halmashauri ya Magu na JSI katika kuboresha mifumo ya Afya na ustawi wa jamii, kutakuwa na mafanikio yafuatayo;-
Baada ya maelezo hayo ametoa mapendekezo kwa Halmashauri kama kama ifuatavyo;-
Mkurugenzi Mtendaji (W) na Mwenyekiti wa Halmashauri wametoa shukrani zao dhati kwa shirika la JSI kwa msaada walio utoa kwa lengo la kusaidia kuboresha utendaji kazi wa wasimamizi wa mashauri ya watoto katika Halmashauri ya magu kwenye kata zilizopewa mafunzo. Aidha wameomba shirika la JSI kuendelea na moyo huo katika utoaji wa huduma kwa wamanchi.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa