Mbunge wa jimbo la Magu Boniventura Kiswaga kupitia mfuko wa jimbo amekabidhi mifuko 120 ya saruji kwaajili ya kuunga mkono nguvu kazi ya wananchi kujenga madarasa sita katika shule ya sekondari Magu Mjini.
Mbunge Kiswaga amekabidhi mifuko hiyo kutekeleza ahadi aliyoitoa wakati akishiriki nguvu kazi ya kuchimba msingi kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Magu Mjini ambapo aliahidi kuchangia mifuko 120 ili kuunga mkono juhudi za wananchi kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mifuko hiyo mratibu wa mfuko wa jimbo Bi. Rosemary Martin Lissu amesema mbunge amekabidhi mifuko hiyo kuunga mkono juhudi za wananchi na kuchangia katika shughuli za maendeleo katika jimbo la Magu.
Aidha amesema mifuko hiyo itumike katika shughuli iliyokusudiwa ili kukamilisha ujenzi wa madarasa hayo ambayo yatatumika na wanafunzi wa Kata ya Magu Mjini.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Magu Mjini , amemshukuru Mbunge kwa kitendo ambacho amekifanya kupitia mfuko wa Jimbo kwa kuchangia saruji mifuko 120 ambazo zitasaidia katika ujenzi wa madarasa sita ya shule hiyo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa