Mbunge wa Jimbo Magu Mheshimiwa Destery B. Kiswaga amewashukuru Watendaji wa Serikali ngazi za Vijiji, Kata Wakuu wa Idara na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Magu, kwa ushirikiano mkubwa waliompatia katika ziara yake jimboni magu ambapo alitembelea kijiji kwa kijiji na kufanikiwa kufanya mikutano 85 ya kibunge jimboni humo. Mheshimiwa Kiswaga amefunguka haya akiwa katika Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 14.11.2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu..
Amesema “Mheshimiwa Mwenyekiti nitumie fursa hii ya baraza lako kuwashukuru sana waheshimiwa Madiwani wote, watendaji wa Vijiji, Kata, Wakuu wa idara zote wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg:Lutengano Mwalwiba kwa ushirikiano mkubwa walionipatia katika ziara yangu, kwa kweli haikuwa kazi rahisi kutembea kijiji kwa kijiji na wakati mwingine nilifanya mikutano mitano kwa siku, na Maandalizi yote waliandaa wao na wananchi walijitokeza kwa wingi kuja kunisikiliza mimi Mwakilishi wao, asanteni na naahidi Mkurugenzi kuna haja ya kufanya tathimini ya pamoja, nitaanda hafla fupi itakayoambatana na mrejesho wa ziara jimboni, Pia ahadi zangu tutaanza kupeleka vifaa na fedha kwa ajili ya miradi hivi karibuni baada ya taratibu kukamilika”.
Mbunge Kiswaga alifanya ziara ya kibunge jimboni kwake ambapo pamoja na mambo mengine alipata fursa ya kusikiliza kero, kutatua kero, kupokea maoni ushauri kutoka wa Wananchi, Ziara hiyo ni utaratibu wa Mbunge aliojiwekea katika kujali wananchi wake kuwa kila Mwaka huwatembelea wananchi, Ziara hiyo ambayo pia ilihamasisha shughuli za mendeleo, kuchangia miradi ya maendeleo jimboni na kuchochea maendeleo kwa ujumla.
Aidha madiwani nao wamemwomba Mheshimiwa Mbunge kuharakisha kupeleka fedha au vifaa ambavyo kupitia ziara yake aliahidi kuchangia kwa ajili ya maendeleo katika kila kijiji. Pia Madiwani nao wamempongeza mbunge kwa utendaji wake na kwamba Wananchi wanapata fursa ya kukutana na Mbunge wao kila mwaka, “Hii imetusaidia hata sisi Madwaini kuwa karibu na Wananchi wetu” amesema Marco Minzi Diwani wa kata ya Bukandwe.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa