Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Wilayani Magu (MASCIINET) imechangia madawati 40 katika shule ya Msingi Chandulu iliyopo Kata ya Ng'haya ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serilkali kuboresha mazingira ya elimu nchini.
Madawati hayo yamekabidhiwa kama sehemu ya ahadi iliyotolewa na mashirika hayo wakati maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Juni 16,2024.
Akizungumza wakati akipokea madawati hayo Katibu tawala wa Wilaya ya Magu Jubilate win Lawuo alipongeza na kushukuru uongozi wa mashirika hayo kwa hatua hiyo muhimu na kusema kuwa mahusiano na ushirikiano kati ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yanaashiria mwanga mzuri , ustawi na ukuaji wa pamoja kwa maendeleo.
Kwa uapnde wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhani ametoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kujitoa Zaidi na kuunga mkono serikali kuendelea kuboresha mazingira ya elimu nchini.
Naye mwakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali Wilayani Magu amesema mpango huo unalenga kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha mazingira ya kujisomea kwenye shule mbalimbali ndani ya Wilaya ya Magu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa