BARAZA la Wafanyakazi Magu limewachagua Lilian Michael kuwa katibu wa baraza pamoja na Allypius Pauliny kuwa katibu msaidizi.

Uchaguzi huo uliosimamiwa na Afisa Kazi wa mkoa wa Mwanza, Peace Felix umefanyika jana tarehe 13 Januari, 2026 katika ukumbi wa halmashauri wa Magu na kushuhudiwa pia na Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri, Mohamed Ramadhani.

Katika zoezi hilo la uchaguzi, jumla ya wajumbe 75 walipiga kura ambapo Lilian alipata kura 55, Allypius kura 19 huku kura moja ikiharibika.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Afisa kazi huyo amewataka viongozi wa baraza hilo kuzingatia sheria ya ajira na mahusiano maeneo ya kazi, kujenga jamii isiyokuwa na matabaka na kuakisi shughuli zinazofanywa na Halmashauri.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa