Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) kwa ngazi ya wilaya ya Magu yamekamilika Mei 20, 2024 katika viwanja vya shule ya Sekondari Magu iliyopo Tarafa ya Itumbili Wilayani Magu .
Mashindano hayo yalianza Mei 16,2024 kwa ngazi ya Shule, Kata, na Tarafa ambapo yalimalizika Mei 20,2024.
Jumla ya tarafa nne ambazo ni Tarafa ya Ndagalu, Sanjo, Kahanagara na Itumbili zilichuana kwenye michezo mbalimbali ili kupata timu ya Wilaya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo Afisa Michezo Wilaya ya Magu Bi. Kabula Malale amesema michezo iiliyoshindaniwa ni pamoja na mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana, mpira wa pete, mpira wa mikono kwa wasichana na wavulana na michezo mbalimbali.
Aidha, alieleza kuwa Michezo hiyo ilikuwa na wanamichezo zaidi ya 400 amabao walichuana katika michezo mbalimbali ili kuunda timu ya Wilaya .
Alisisitiza kuwa Michezo huimarisha afya na serikali imeweka juhudi kubwa kuendeleza michezo mashuleni ili kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi na tasnia ya michezo kwa ujumla.
Baada ya kukamilika kwa michezo hiyo kwa ngazi ya Wilaya hatua inayofuata ni kuwekwa kwa kambi maalum ya wachezaji na washindi waliopatikana kwaajili ya kupata wawakilishi wataowakilisha Wilaya katika ngazi ya mkoa .
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa