ZAIDI ya makarani 600 wa vituo vya uchaguzi jimbo la Magu mkoani Mwanza wameapishwa leo Jumamosi na kupewa semina maalumu kwa ajili maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Makarani hao ambao kundi moja limekusanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Kisesa na la pili shule ya sekondari Mugini mjini Magu, wamehimizwa kuzingatia viapo vyao, sheria kanuni na taratibu zilizowekwa na tume huru ya uchaguzi ili kuhakikisha wapiga kura wanapata haki zao za msingi kwa mujibu wa katiba.
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi jimbo la Magu, Josephat Mbura pia ametoa wito kuzingati mafunzo waliopatiwa ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao ya msingi.

Wakizungumza katika mafunzo ya kuongoza wapiga kura siku ya uchaguzi baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Mmoja wa Makarani hao, Halima Abdalah ameahidi kutii na kusimamia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na tume huru ya uchaguzi.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa