Mkuu wa wilaya ya Magu Mhe. Rachel Kassanda amewataka wazazi wilayani Magu kuhakikisha wanapeleka watoto wao katika vituo vya afya kupatiwa chanjo ya Surua na Rubella ili kuepuka madhara yanayowezajitokeza ikiwa mtoto hatopata huduma hiyo mapema.
Agizo hilo amelitoa Februari 15,2024 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chanjo iliyofanyika katika hospitali ya wilaya ya Magu ambapo wazazi na walezi mbalimbali walijitokeza kupeleka watoto wao kupata chanjo hiyo.
Aidha ameitaka timu ya wataalamu iliyoundwa kwaajili ya zoezi hilo kuhakikisha wanahamasisha wananchi ili kufikia lengo lililowekwa na serikali.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Magu amesema kuwa zoezi la utoaji wa chanjo litafanyika katika Vituo vya Afya,zahanati,shule za Msingi na maeneo mengine yaliyoanishwa katika Vijiji na Kata kulingana na mahitaji.
Amesema chanjo hiyo ni muhimu sana hivyo ni vema kuhakikisha hakuna mtoto atakayekosa chanjo, kwani kwa hali ya kawaida unaweza ukaona haina maana lakini ukaja kupatwa na madhara baadaye.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa