Halmashauri ya Wilaya ya Magu imepongezwa katika kutumia mifumo ya Tehama kwenye utoaji wa huduma za kijamii ambayo yamerahisisha huduma hizo katika sekta ya Afya, Elimu na maendeleo ya jamii.
Pongezi hizo zimetolewa na timu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo iliambatana na wadau wa maendeleo ( USAID) wakati wa ziara kwaajili ya kukagua mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma ( PS3+) ambao unatekelezwa katika Wilaya ya Magu.
Katika Ziara hiyo timu hiyo ilitembelea shule ya Sekondari Nyanguge ambapo ilikagua namna ambavyo shule hiyo inatumia Tehama katika kutekeleza shughuli mbalimbali pamoja na kusikiliza changamoto na mapendekezo ili kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa kutumia mifumo ya Tehama.
Aidha timu hiyo ilitembelea kikundi cha wajasiriamali wanawake cha ' JIRANI AMEKUAJE ' ambapo ilikagua mfumo wa usimamizi wa utoaji wa mikopo itokanayo na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ITPLMIS ( Ten Percent Loan Management Information System) .
Wakiwa katika kikundi cha Jirani amekuaje walisikiliza changamoto za matumizi ya mfumo huo kwa wanufaika pamoja, kupokea mapendekezo kwaajili ya kuboresha mfumo pamoja na kusikiliza faida zilizopatikana tangu mfumo huo uanze kutumika.
Pia timu hiyo ilitembelea kituo cha Afya Kisesa ambapo walikagua matumizi ya mfumo wa GoTHOMIS .
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa