Halmashauri ya Wilaya ya Magu ya imepokea vifaa vya kwa shule 28 za awali zilipo Wilayani humo kupitia mradi wa BOOST kwa lengo la kuboresha elimu ya awali katika mazingira ya kufundishia na kujifunzia na kumudu stadi za (KKK) Kusoma, kuandika na kuhesabu .
Vifaa hivyo vimepokelewa na walimu wa shule za msingi 28 zilizopo wilaya ya Magu ambazo zinatarajiwa kunufaika na vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kuongeza uelewa wa wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Afisa Elimu Takwimu na Vifaa (SLO)Wilaya ya Magu , Jackson Buhatwa amesema shule zilizonufaika na vifaa hivyo ziwe chachu kwa kutimia zana za ufundishaji walizopokea kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wa shule zilizopokea vifaa hivyo Mwalimu Gwanchele wa shule ya msingi Bugabu ameishukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt. Samia kwa kutoa vifaa hivyo na kuahidi kuwa vitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa kuboresha mazingira ya elimu ya awali.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa