Wananchi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Magu , wadau wa maendeleo, wataalamu, viongozi wa vyama vya siasa wamejitokeza kwa wingi katika Kongamano la cha kuchangia Maoni yao katika Mpango wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 - 2050.
Kongamano hilo Liliwakutanisha Wananchi kutoka Makundi mbalimbali ili kutoa Maoni yao juu ya Tanzania waitakayo kwa Miaka ya baadae.
Kongamano hilo limefanyika Julai 29, 2024 katika viwanja vya sababasaba ambapo mgeni rasmi na mwenyekiti wa kongamano alikua ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Magu Jubilate win Lawuo ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Joshua Nassari.
Akizungumza wakati akifungua kongamano hilo DAS Lawuo amesema kuwa maoni wa wananchi ni muhimu sana katika maandalizi ya dira hiyo na kusisitiza kuwa Serikali itayafanyia kazi Maoni yote ya Wananchi ili kuwa na Mpango wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 - 2050 ulioshirikisha Wananchi Wote.
Aidha amewataka wadau wa Maendeleo na Wananchi kujikita katika kutoa maoni yenye manufaa kuhusu Mwelekeo wa maendeleo wanayotaka kuyafikia ifikapo 2050.
Wakizungumza wakati wa kongamano hilo baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Magu wameipongeza serikali kwa kuandaa kongamano hilo na kubainisha kuwa watatoa maoni yenye tija ili kurahisha mchakato wa maandalizi ya dira hiyo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa