Wazazi Wilayani Magu wamehimizwa kutambua umuhimu wa chakula kwa afya ya mtoto, kuwa ndicho kinachojenga akili, mwili na saikolojia ya mtoto, hivyo wameombwa kuchukulua umuhimu mkubwa jambo hilo kwa kuunga mkono zoezi la kuchangia chakula shuleni kwa ajili ya umuhimu wa Lishe Bora na ufaulu wa watoto.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Magu Jubilate win Lawuo wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Kitaifa yenye kauli mbiu " Lishe Bora kwa Vijana Balehe, Chachu ya Mafanikio Yao" kwa Wilaya ya Magu ambayo yaliambatana na uzinduzi wa kampeni ya lishe kwa vijana balehe yaliyofanyika katika shule za ya Msingi Nyalikungu Leo Jumatatu Oktoba 30, 2023.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Katibu Tawala huyo amesema suala la chakula ni muhimu sana ba lazima lizingatiwe ili wanafunzi waweze kusoma kwa ufanisi wawapo shuleni.
" Hii itasaidia kuinua ufaulu wa wanafunzi na kuimarisha mahudhurio yao kwani wanafunzi wengi wamekua wakitoroka shuleni kwaajili ya kwenda nyuma kula chakula hivyo ni vyema wazazi tukaona umuhimu na kuunga mkono suala hili" amesema
Aidha Katibu Tawala Lawuo amewahimiza wananchi kuzingatia mlo kamili na kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta, sukari, na chumvi kwa wingi mfano Chipsi, soda, Pizza, Biskuti, keki, na mikate ya unga mweupe,soda, juisi zilizoongezewa sukari, na vyakula vya kukaanga ikiwemo mihogo, viazi, nyama kwani itasaidia Kuepuka unene/uzito kupita kiasi, magonjwa ya moyo, kiharusi, shinikizo la juu la damu, saratani, kisukari na ugonjwa wa figo sasa na baadae.
Kwa upande wake Afisa Lishe Wilaya ya Magu Bi Magdalena G. Lema amesema Magu ni miongoni mwa halmashauri nchini zinazotekeleza afua za lishe ili kutokomeza/Kupunguza changamoto mbalimbali za lishe kwa mama mjamzito, watoto chini ya miaka mitano
"leo tunazindua rasmi mkakati wa kutokomeza/kupunguza changamoto za lishe kwa vijana balehe ili kufikia kiwango ambacho si tatizo katika jamii kwa utaratibu wa kutoa elimu na kupima hali za lishe za vijana balehe(miaka 5-19)" amesema
Kuhusu mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa mpango wa Lishe Kitaifa Wilaya ya Magu imfanikiwa kupunguza hali ya ukondefu kwa watoto wa chini miaka mitano kutoka 3.5% Hadi 2.8% .
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa