Wazazi na walezi wametakiwa kuweka tofauti zao pembeni na kushirikiana katika suala la malezi ya watoto ili kuwanusuru watoto katika mnyororo wa mmomonyoko wa maadili kwani msingi wa malezi na maadili ya binadamu yanaazia kwenye msingi wa familia.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Joshua Nassari wakati wa maadhimisho ya siku ya familia duniani Mei 15,2024 yaliyofanyika katika Kata ya Nyigogo Wilayani Magu.
“Matatizo ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na wazazi na walezi ambapo tafaouti zao zimekua zikiathiri watoto hivyo wekeni pembeni tofauti za kidini, kikabila na migogoro binafsi na mshirikiane katika malezi bora ya watoto kwa kuwa wenye jukumu hilo ni wazazi ”.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mh.Simon Mpandalume amesema Malezi bora katika familia ndio msingi wa malezi kwa watoto katika jamii yetu hivyo wazazi wanapaswa kuzingatia kutoa malezi bora kwa watoto ndani ya familia na jamii kwa ujumla ili kuwa na taifa lenye uchu wa kujiletea maendeleo.
Naye Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Magu amesema idara ya maendeleo ya jamii imeendelea kutoa elimu ya malezi na makuzi katika ngazi ya jamii katika kuanzia vijijini hadi ngazi ya kata kuelimisha jamii kuhusu malezi na makuzi.
Siku ya Familia Duniani inaadhimishwa kila Mei 15, 2018 na kwa mwaka huu inaadhimishwa ikienda na kaulimbiu isemayo “Tukubali Tofauti Zetu Kwenye Familia, Kuimarisha Malezi ya Watoto.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa