Katibu tawala wa Wilaya ya Magu Jubilate win Lawuo amewataka wananchi wa Magu kuendeleza utamaduni wa kupanda miti na kutoitelekeza miti iliyopandwa ili kutunza mazingira na kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Katibu Tawala Lawuo ametoa wito huo wakati akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika shule ya sekondari Kigangama iliyopo Kijiji cha Kigangama kata ya Kitongosima Wilayani Magu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanzania.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo katibu tawala huyo amesema kupanda miti ni muhimu katika utunzaji wa mazingira, kupata vivuli, hewa safi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
" tutakapokua na miti mingi katika Wilaya yetu Itakua nzuri na mazingira yatakua mazuri hatutopata janga la njaa, upepo mkali wa kuezua majengo na hali nzuri ya hewa" amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu Fidelica G. Myovella amewataka wananchi wanaozunguka maeneo yaliyopandwa miti hiyo kuendelea kuitunza ila kuifanya Magu kua na mazingira safi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa