Halmashauri ya wilaya ya Magu imeshika nafasi ya kwanza katika Maonyesho ya Wakulima Nanenane katika viwanja vya maonesho Nyamhongolo – Mwanza leo tarehe 08.08.2019. katika Maonyesho hayo, kweye kundi la Halmashauri, Magu DC imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Nyang’hwale DC iliyoshika nafasi ya pili na Ilemela MC imeshika nafasi ya tatu.
Pia katika kundi la wakulima, Magu DC imeshika nafasi ya kwanza kwenye kilimo cha pamba, Mbogwe DC nafasi ya pili kwenye miche ya matunda na Kwimba DC imeshika Nafasi ya tatu kwenye zao la Mpunga. Kwa Kundi la wajasiriamali, mfugaji bora ni Japhary Omary kutoka Magu kwa ufugaji wa Ndege wa aina mbalimbali.
Ushindi huu ni kutokana na ushirikiano baina ya Viongozi (DC, DED, na Wakuu wa Idara na Vitengo) na watumishi walioshiriki kikamilifu katika maonyesho hayo. Aidha Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. Lutengano G. Mwalwiba amekabidhiwa kombe la ushindi kwa niaba ya watumishi wote.
Halmashauri ya Magu imeshiriki kikamilifu katika maonyesho ya bidhaa mbalimbali za kilimo Mifugo na Uvuvi ambapo Kaulimbiu kwa mwaka 2019 inasema “ Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa Nchi” Maonyesho hayo ya Nanenane yalianza tarehe 01.08.2019 na kuhitimishwa rasmi tarehe 08.08.2019.
“MAGU: KUSEMA NA KUTENDA, KAZI NA MAENDELEO”
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa