Wananchi wa Wilaya ya Magu wamejitokeza kwa wingi kupata huduma za afya kutoka kwa madaktari bingwa wa Rais Dkt. Samia waliowasili wilayani humo kutoa huduma za kibingwa kuanzia Oktoba 22 hadi Oktoba 24 2025.
Huduma hizo zimeendelea kuwagusa wananchi kutoka maeneo mbalimbali, huku wengi wakieleza kufurahishwa na ukaribu na weledi wa madaktari hao.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Daktari bingwa wa magonjwa ya Watoto Dkt. Rehema Tagalile amewataka wananchi wa Magu na maeneo ya Jirani kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo adhimu kupata vipimo na matibabu, hasa kwa wale wanaosumbuliwa na magonjwa sugu au waliokosa huduma za kibingwa kwa muda mrefu.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Dkt. Raphael J. Mhana ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia kwa kuratibu ujio huo kupitia Wizara ya Afya, akieleza kuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wengi ambao wamekuwa na changamoto ya kufuata huduma mbali
Alisisitiza kuwa ofisi yake itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa