Halmashauri ya wilaya ya magu imekuwa miongoni mwa Halmashauri za kanda ya ziwa katika maadhimisho ya siku ya wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyamhongolo Mkoa wa Mwanza. Bidhaa mbali mbali zinazotokana na kilimo na mifugo zimeonyeshwa katika maonyesho hayo tangu tarehe 1-8/08/2017. Kauli mbiu ya maonyesho hayo ni "Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kufikia uchumi wa kati".
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa