kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya magu kimefanyika leo tar 28/10/2022 katika ukumbi wa CCM wilaya lengo la kikao hicho lilikuwa ni kupitia na kujadili miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo Akizungumza katika kufunga kikao hicho mwenyekiti wa halmashauri hiyo MH SIMON MPANDALUME pamoja na kuwapongeza watendaji na madiwani kwa kusimamia vyema miradi hiyo lakini aliomba kuendelea na kasi hiyo katika miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa akitolea mfano katika robo ya kwanza Halmashauri imetoa millioni 220.5 katika kata 13 kati ya 25 kukamilisha miradi mbalimbali iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi hivyo nivyema kusimamia vizuri ili fedha hizo zikatekeleze malengo yaliyokusudiwa
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa