Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Magu (DCC) Imekutana katika kikao maalum cha kushauri Rasmu ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Akiongoza kikao hicho Mwenyekiti wa DCC ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Mwalimu Khadija Nyembo, amewaomba wajumbe kuishauri serikali kwa busara, “ushauri wenu ni tija kwa Maendeleo ya wilaya yetu” amesisitiza Mwl. Khadija Nyembo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu, Lutengano Mwalwiba amesema kuwa Rasimu hii ya Bajeti imezingatia Dira ya maendeleo ya Taifa kufikia 2025. Mpango wa pili wa miaka mitano wa Taifa. Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ya 2015-2020,
Pamoja na Mambo mengine Bajeti hiyo imejikita katika kuleta matokeo chanya na yenye kugusa maisha ya Wananchi mmoja mmoja, Pia Bajeti, imejikita katika Miradi inayolenga kuzingatia malengo endelevu 17 ya mwaka 2030. Pia imezingatia Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli aliyolihutubia Bunge wakati akilizindua Mwezi Novemba, 2015, aidha ameieleza kamati kuwa Halmashauri inatarajia kutumia 44,053,595,000.00 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
vipaumbele kumi vimeanishwa katika Rasmu ni kama ifuatavyo;-.
Kuongeza mikakati ya kimiradi ili kuongeza mapato ya Halmashauri, kama vile ;-
kujenga stendi ya Magari makubwa ya Mizigo Kisesa.
Ujenzi wa Stand ya Hiace Kisesa na Nyanguge,
Ujenzi wa scheme mbili za Kilimo cha Umwagiliaji, Sawenge na Mwamibanga.
Ujenzi wa Chuo cha ufundi VETA -Ilungu.
Ujenzi wa shule ya Bweni ya Wasichana.
Ujenzi wa shule za sekondari za kidato cha 5 na 6.
Kuajili watumishi wapya 1,404
Ukamilishaji wa nyumba za walimu wa shule za Msingi.na sekondari.
Wajumbe wa kamati ya ushauri nao wamepata muda mzuri na kushauri maeneo mbalimbali katika Rasmu ya Bajeti, Hivyo kikao kimekuwa na mafanikio makubwa zaidi kwani Bajeti inaaksi pia fursa kwa vijana na Wanawake. Rasimu hiyo ushauri wa DCC Utafikishwa kwenye kamati za kudumu za Halmashauri pamoja na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Magu.
Kikao kimehudhuriwa na Viongozi wa Vyama vya siasa, Viongozi wa Sekta binafsi, Wakuu wa idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata zote, Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya Magu, Ndg. Menruf F. Nyoni, Mkurugenzi Mtendaji (W)(DED) ambaye ni katibu wa kikao hicho na Mkuu wa Wilaya (DC) ambaye pia ni mwenyekiti.wa kikao hicho.
“Kwa pamoja tunajenga Magu yetu”
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa