Mkuu wa Wilaya ya Magu Dkt. Philemon Sengati leo tarehe 22.01.2019 ameongoza kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya (DCC) kupitia nakushauri Rasimu mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/2020, Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya aliyewakilishwa na Afisa Mipango, Mwenyekiti wa Halmashauri Hilali Elisha, Viongozi wa vyama vya siasa, Wakuu wa Idara, Maofisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, akiwakaribisha wajumbe katika kikao hicho maalum cha kujadili bajeti, ameshukuru wajumbe kwa mahudhurio na kuwataka kuwa huru katika kupitia na kujadili mapendekezo ya bajeti, amesisitiza kuwa wazalendo katika kujadili mapendekezo haya ya bajeti kwa ajili halmashauri yetu.
Akiwasilisha rasimu ya bajeti Kaimu Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Emmilian Makomelelo amesema kuwa Halmashauri ya Magu inaomba kuidhinishiwa 50.9 bilioni kutoka vyanzo vyake mbalimbali na kutoka Ruzuku ya Serikali kuu. “Rasimu ya bajeti imejikita katika miradi inayolenga kuzingatia malengo endelevu 17 ya mwaka 2030 (SDGs), pia miradi hiyo imelenga kuleta matokeo chanya na yenye kugusa maisha ya Wananchi moja kwa moja”amesema Makomelelo
Rasimu ya Bajeti imeanisha vipaumbele vya bajeti,ambavyo ni pamaja na kuanzisha Stand ya Hiace Kisesa, Nyanguge na kabila, Ukamilishaji wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu kwa shule za Msingi na Sekondari, Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) Katika Hospital ya Wilaya ya Magu, Ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati, Ukamilishaji wa miradi maji na uchimbaji wa visima, Kupunguza uhaba wa watumishi kwa kuajiri watumishi wapya 1481, katika kada za Afya, Elimu, Wahasibu, Kilimo, Usatwi wa jamii utawala na kada zingine.
Wajumbe wa kikao hicho wamepata nafasi ya kujadilikwa uwazi rasimu ya bajeti, wameshauri miradi viporo ya muda mrefu ipewe kipaumbele katika mwaka huu, ambapo Idara ya Afya imeanisha kukamilisha ujenzi wa zahanati 16 za Nsola, Nyang’hanga, Inolelo, Igombe, Matela, Lutale,Isangijo, Ikengele, Shishani,Nyashigwe, Salong’we, Shinembo, Kitumba,Ihayabuyaga, na Langi.
Kwa kauli Moja wajumbe wameridhia kupitisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2019/2020 katika Halmashauri ya wilaya ya Magu kama ilivyopendekezwa.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa