Kamati ya fedha , Uongozi na mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Magu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Simon Mpandalume imefanyika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Mwaka wa fedha 2023/2024.
Ziara hiyo imefanyika Leo Jumamosi Oktoba 28 ambapo kamati hiyo ikiambata na wajumbe na wakuu wa idara mbalimbali za Halmashauri walitembelea miradi Saba ikiwemo ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Misungwi Kata ya Buhumbi, Ujenzi wa zahanati ya Iseni kata ya Sukumu , ujenzi wa nyumba vitatu vya maabara katika shule ya Sekondari Masengese kata ya Jinjimili na miradi mingine inayotekelezwa na Halmashauri hiyo .
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya fedha, Uongozi na na utawala Mh. Simon Mpandalume amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Magu kwa kuendelea kuanzisha miradi ya maendeleo katika maeneo yao ikiwemo kujenga maboma ya shule na zahanati na kusisitiza kuwa Wananchi kuendelea kua na umoja na mshikamano kuanzia miradi kwani serikali itaendelea kupeleka fedha kwaajili ya ukamilishaji wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Bi Fidelica G. Myovella amesema serikali itaendelea kupeleka fedha kwaajili ya kukamilisha miradi yote iliyoanzishwa kwa nguvu za Wananchi kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ili kuleta maendeleo katika Wilaya ya Magu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa