Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angelina Mabula alipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Magu tarehe 28.07.2017 ili kuepuka migogoro ya Ardhi. ameagiza kuwa, wananchi waelimishwe kuhusu matumizi bora ya ardhi,sheria za ardhi na kuepuka migogoro ya ardhi katika maeneo yao.
Aidha amesisitiza kuwepo suala la urasimishaji wa ardhi katika Wilaya, na Halmashauri iwe na mipango ya muda mrefu kwa kuandaa ‘Master Plan’. Halmashauri inapotwaa ardhi kutoka kwa Wananchi ilipe fidia kwa wakati ili kuepusha migogoro na Wananchi.
Amesema kila robo ya Mwaka lazima kodi ya ardhi inayolipwa, taarifa yake itolewe jinsi fedha zinavyokusanywa. Wananchi wafuatiliwe waweze kulipa kodi kwa wakati ili Serikali ipate Mapato. Katika maeneo ya Vijijini, upimaji wa ardhi ufanyike na wananchi wapewe hati miliki za kimila kwani kwa kufanya hivyo ardhi yao inaongezeka thamani. Aidha ametoa maelezo kuwa Halmashauri ya Wilaya ina watumishi wa Idara ya Ardhi wa kutosha, kinachohitajika ni kufanya kazi kwa bidii ili ardhi ipimwe. Elimu itolewe kwa wenyeviti wa vijiji waache kuuza ardhi kiholela.
Ameagiza Mabaraza ya Ardhi ya kata yapewe elimu ya kusimamia kesi za ardhi zinazojitokeza. Pia Halmashauri itumie Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuweka Mandhari mazuri ya mji kwa kuwapatia maeneo ya kujenga Nyumba.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa