Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yaMagu Lutengano George Mwalwiba, akiwa ni Mgenirasmi amezindua mafunzo ya ukusanyaji wa takwimu za uvuvi katika ziwa Victoriakwa kutumia mtandao wa simu za kiganjani. Mafunzo hayo ambayoyamefanyika wilayani Magu na kuwahusisha maafisa uvuvi na wakusanyaji takwimuza mavuvi kutoka Wilaya za Misungwi,Buchosa,Sengerema, Nyamagana, Ilemela, Magu,Busega, Bunda, Ukerewe, Butiama, Musoma mjini na vijiji, Rorya na Tarime.Watalaam kutoka kituo cha utafiti wa uvuvi mkoa wa Mwanza, Watalaam wa taasisi ya utafiti wa uvuvi Tanzania(TAFIRI) pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uvuvi Tanzania Bwana Mayala Philipo.
Mafunzo yaliandaliwa na Taasisi ya utafiti wauvuvi Tanzania(TAFIRI) chini ya Wizara ya mifugo na uvuvi, Lutengano Mwalwibaamewataka watendaji wakuu wa idara ya uvuvi kufanya kazi kwa weledi, “Katikazama hizi ndugu zangu utapimwa kwa kile ulichofanya hizi siyo zama zaubabaishaji twendeni tukafanye kazi kwa bidii na mipango madhubutiitakayosaidia Serikali yetu kukusanya mapato ya kutosha kupitia sekta hii nyetiambayo inachangia pato kubwa la Serikali”, Amesema Lutengano DED Magu.
Pamoja na kuzindua mafunzo Lutengano pia amekabidhisimu kwa maafisa uvuvi wa wilaya zote 13, waliohudhuria, amesema kuwa “ lazimasasa tuwe wakweli mfumo huu wa ukusanyaji wa takwimu za uvuvi kwa njia yamtandao unaweza kukuumbua maana unasoma mpaka mahali ulipo, lakini utarahisishakukusanya taarifa sahihi na kwa wakati, hivyo tumieni taaluma zenu kulindaheshima zenu za kitaaluma na kutoingiliwa na watu wengine wasiokuwa wanataalumawa eneo lenu, zitendeeni haki taaluma zenu hizi simu ni mali ya Serikalimkazitumie kwa kazi iliyokusudiwa na kwa uadilifu”.
Awali Afisa uvuvi Wilaya ya Magu Tausi Kiulaakiwa ni mwenyeji wa Mafunzo hayo, ameshukuru Wizara kwa kuleta mfumo waukusanyaji takwimu kwa njia ya simu, “Hii itatusaidia kupata takwimu sahihi nakwa muda muafaka na kwa namna ya pekee itaondoa zana ya kupika takwimu kamailivyokuwa hapo awali. Lakini kwa hatua hii mpya tunaamini kuwa baada yamafunzo haya tutakwenda kuokoa mapato ya uvuvi yaliyokuwa yakipotea kutokana naukosefu wa takwimu sahihi za wavuvi”.
Dr. Onyango (UDSM) kitengo cha utafiti wa uvuvi amesemakuwa Serikali imekuwa ikipata 48% ya mapato na uvuvi kwa mfumo uliokuwepo waanalogia, lakini sasa kupita mfumo mpya wa mtandao Serikali itaokoa mapato yauvuvi kwa 52% ambayo kila mwaka yalikuwa yakipotea. Pia Mwalikishi waMkurugenzi wa Uvuvi Tanzania Bwana Mayala Philipo amesema kuwa Wizara ya uvuviimekuja na huu mfumo baada ya tafiti za kutosha kuwa ilikuwa inakosa takwimusahihi kutoka katika wavuvi wote kwa maana ya maziwa na bahari, “Lakinitunaimani kuwa mfumo huu utaiwezesha Wizara kufikia malengo yake ya kukusanyamapato kwa halisi lakini kujua hali halisi ya wavuvi nchini. Mmoja wa wakufunziwa mfumo amesema kuwa mfumo huo unatumia gharama nafuu ni kama Tshs 500/- kwawiki hivyo serikali itatumia kiasi kidogo sana kukusanya mapato makubwa zaidina kila taarifa itaingia mojamoja kwenye kanzi data ya wizara. Hakutakuwa nausumbufu wa kukusanya fomu za takwimu.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa