Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Lutengano George Mwalwiba, leo tarehe 05.06.2019 ametoa msaada wa runinga moja yenye thamani ya Shilingi milioni moja na laki nne kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wanasoma katika wa shule ya msingi Itumbili.
DED Lutengano amewaeleza Walimu na Wazazi wa watoto wenye mahitaji maalum kuwa, Mwaka jana alipata nafasi ya kuwaandalia chakula na kula pamoja wanafunzi , ambapo kupitia hafla hiyo aliahidi kuwanunulia Runinga moja kwa ajili ya kuangalia na kufundishia, “Hivyo leo Mungu amenibariki natimiza nadhili hii kwa Mungu na kwenu ninyi wanangu mnasoma hapa, Kwani katika maandiko matakatifu imeandikwa kuwa ‘ Waweza kumjaribu Mungu kwa Matoleo”
Aidha Lutengano amemshukuru Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Magu Mhe Kiswaga kwa kununua king’amuzi cha azam ambacho kitawezesha Runinga hiyo kufanya kazi kuanzia leo, pia ameahidi kuwa ataendelea kulipa ankala yake kila mwezi. Vilevile ametoa wito kwa jamii kuacha kuficha watoto wenye mahitaji maalum bali wawalete shuleni. Pia amewapongeza Walimu wote wa shule ya Msingi Itumbili kwa kazi yao nzuri ya kuwalea na kuwahudumia watoto hao kwa upendo mkubwa.
DED Lutengano ameambatana Mganga Mkuu Dr.Maduhu, Mchungaji Maliganaya wa KKKT-Magu, Afisa mipango Wilbard Bandola, Afisa Ustawi wa Jamii Coretha Sanga, Ridhiwan Shukuma -Mweka hazina, wakuu wa Idara hao nao wamemuunga mkono Mkurugenzi ambapo Dr.Maduhu na Afisa mipango wamejitolea kuwalipia wanafunzi wote bima ya afya, Huku Mweka hazina na Afisa Ustawi wao wamejitolea kununua vyerehani viwili ikiwa ni moja mahitaji makubwa kwa wanafunzi hao. Huku Mchungaji Maliganya ameahidi kilo 60 za mchele mapema watakapofungua shule.
Mwalimu Mkuu wa Rhobiry Chacha amempongeza Mkurugenzi pamoja na wakuu wa Idara kwa upendo wake wa pekee na moyo wa utoaji sadaka zenu hizi, Hakika Mungu awatapa thawabu yake, Pia Runinga hii itatusaidia sana kuwafundishia watoto wetu hawa wenye mahitaji maalum, kwani Walimu walikuwa wanahangaika kuweka masomo kwenye kompyuta zao mpakato na kuanza kuzunguka kuwaonesha wanafunzi lakini Sasa hii Runinga ya inch 43, itarahisisha sana ufundishaji na itachochea kuongeza ufaulu.
Akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi Bahati Chacha darasa la sita ambaye ni mlemavu wa macho, amemshukuru na kumpongeza Mkurugenzi mtendaji kwa moyo wake wa kuwajali , na hata Mwaka jana alikuja tulijumuika naye, Sisi tunampongeza sana kwa hii Runinga itatuwezesha kupata habari mbalimbali pia tunaoishi hapa itakuwa ni ya msaada sana kwetu, Kwani hatukuwa tukipata habari muda wote , Tumashukuru na Mungu azidi kumbariki kwa upendo anaotutendea ni Kiongozi anayejitoa na amedhamiria kusaidia jamii vizuri hasa sisi walemavu.
Magu kazi na maendeleo =Kusema na kutenda
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa