Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhani ametembelea kambi ya vijana wa shule ya msingi iliyopo shule ya msingi Isandula ambayo ina wanafunzi 121 ambao wanatarajia kuiwakilisha Wilaya ya Magu katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa yanayoshirikisha michezo ya mpira wa miguu kwa wanawake na wanaume, kikapu mpira wa Pete, riadha, kwaya, ngoma na mingineyo.
Akizungumza wakati alipotembelea kambi hiyo amewataka viongozi, wahudumu wa afya na makocha wa timu hizo kuendelea kuwasimamia wanafunzi hao waweze kufanya vizuri katika michezo na kuweza kuwakilisha vyema katika mkoa na ngazi ya Taifa watakapo chaguliwa.
Aidha ameahidi kwa wale watakaochaguliwa kuendelea na mashindano kwa hatua za mbele zaidi kutakuwepo na zawadi ya motisha kwa washindi huku akiwakumbusha kwamba wahakikishe wanashinda michezo yote.
"Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kuhakikisha ina vilea na kuviendeleza vipaji mlivyo navyo, muhimu ni kujitahidi mtakao tuwakilisha mrudi na ushindi mkubwa na sio kusindikiza wenzetua” amesema.
Kwa upande wake wake Afisa Elimu elimu ya awali ya awali na msingi Wilaya ya Magu Bi. Glory Mtui amesema wachezaji wote 121 wana afya nzuri na maandalizi yanaendelea vizuri na ameahidi Magu itafanya vizuri katika zote za mashindano hayo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa