Katika kuelekea Sherehe za Kilele Cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano, leo Aprili 25,2024 Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh Joshua Nassari amezindua mashindano ya michezo mbalimbali yenye lengo la kushajaisha na kupamba shamrashamra za Maadhimisho hayo.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo yaliyofanyika kweye Viwanja vya Mwanankanda Kata ya Magu Mjini DC Nassari amesema mashindano hayo ni muhimu kwa kudumisha Muungano lakini pia ni sehemu ya kukuza michezo na kuibua vipaji.
Michezo iliyochezwa ni Mpira wa Miguu kwa wavulana na wasichana, mpira wa wavu, pamoja na Mashindano ya ngoma.
Katika mpira wa Miguu kutakua na mchezo kati ya Shule ya Sekondari Magu na Itumbi pamoja na Timu ya Watumishi wa Wilaya ya Magu dhidi ya Umoja FC.
Kwa upande wa mpira wa Pete kutakua na mchezo kati ya Shule ya Sekondari Nyanguge na Itumbili Sekondari.
Baada ya michezo hii shamrashamra za muungano zitahamia katika Uwanja wa Sabababa ambapo utafanyika mkesha ambao utaambatana na burudani mbalimbali za muziki wa kizazi kipya , ngoma za asili na burudani nyinginezo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa