Wadau na wanunuzi wa zao la pamba wametakiwa kushiriki katika kuongeza uzalishaji na tija kwenye zao la pamba kwa kutoa michango mbalimbali kwasababu wao ni wadau muhimu katika maendeleo ya zao hilo na si wakulima pekee.
DC Nassari ametoa rai hiyo wakati wa kikao cha kamati ya mazao ya wilaya kwaajili ya kutathmini zao la pamba katika ununuzi wa zao hilo kwa msimu huu wa Kilimo kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa Wilaya.
Akizungumza na wanununuzi wa zao la pamba DC Nassari amewataka wakulima, AMCOS na wanunuzi wa zao hilo kushirikiana na kua kitu kimoja wanapokutana na changamoto, kero na matatizo katika kipindi Cha ununuzi wa pamba.
Aidha DC Nassari amewataka viongozi wa AMCOS kufanya kazi kwa weledi ili kuleta usawa katika makampuni yanayonunua pamba katika Wilaya yote ya Magu ili msimu unapofungwa kusiwepo na deni lolote kutoka kwa makampuni au mkulima.
Pia amewataka wataalamu wa kilimo Wilayani Magu kuendelea kutoa Elimu kwa wakulima wa zao la pamba kuzingatia taratibu za kilimo cha zao hilo ili kuongeza tija na uzalishaji na kuacha kilimo cha mazoea.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Magu. Haki zote zimehifadhiwa